Home Makala Yanga sc Yafungiwa Tena

Yanga sc Yafungiwa Tena

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefungiwa kusajili na shirikisho la soka duniani (FIFA) mpaka pale itakapomlipa fedha zake za usajili mchezaji Gael Bigirimana ambapo mchezaji huyo alishinda kesi baada ya kushtaki Fifa.

Yanga sc walipaswa kumlipa mchezaji huyo ndani ya siku arobaini na tano tangu kutolewa kwa hukumu hiyo lakini klabu hiyo haikutekeleza hivyo kuwalazimu Fifa kufikia hatua hiyo ya kuwafungia kufanya usajili mpaka pale watakapolipa.

Yanga sc walimsajili Bigirimana na kumtambulisha kwa mbwembwe kubwa wakati wa mkutano mkuu misimu msimu 2021/2022 lakini baada ya michezo kadhaa mwalimu Nasredine Nabi aliamua kumuweka benchi kutokana na kuwa na kiwango duni.

banner

Hata hivyo baadae Yanga sc waliliondoa jina la mchezaji huyo katika usajili wa ligi kuu kutokana na kusajili zaidi ya wachezaji wa kigeni 12 wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni hivyo staa huyo aliwekwa pembeni huku ikisemekana kuwa alikua akilipwa mshahara kama kawaida ispokua hakua amemaliziwa hela ya usajili.

Wakati wa kambi ya mwanzoni mwa msimu mchezaji huyo aliwasili kambini hapo kuangalia kama ataendelea kupata nafasi lakini mpaka sasa haonekani kikosini humo ishara kwamba tayari mambo sio mazuri baina yao japo ana mkataba wa mwaka mmoja ambao utamalizika mwishoni mwa msimu huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited