Msafara wa mastaa wa klabu ya Yanga sc jana ulifanikiwa kuwasili Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Rayon Sports ya nchini humo utakaofanyika siku ya kesho ijumaa agosti 15 kuadhimisha siku maalumu ya klabu ya Rayon maarufu kama Rayon’s day.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Amahoro nchini humo ambapo mastaa wa klabu ya Yanga sc wanatarajiwa kuamsha shoo ya maana uwanjani ili kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo ndani na nje ya nchi ambao wanatamani kuwaona mastaa mbalimbali waliosajiliwa klabuni hapo.
Katika msafara huo ambao umesafiri wamo mastaa wote wa kigeni waliosajiliwa msimu huu na kikosi cha mabingwa hao ambao wataonekana kwa mara ya kwanza siku hiyo.
Uwepo wa mastaa hao nchini humo umeamsha shangwe katika mitaa mbalimbali jijini Kigali ambapo idadi kubwa ya mashabiki walijitokeza kuwapokea kuanzia uwanja wa ndege hali ambayo iliwashangaza wachezaji wageni pamoja na kocha Roman Folz ambaye alishangaa klabu hiyo kuwa na mashabiki mpaka nje ya nchi.
Katika ratiba ya klabu hiyo nje ya uwanja imetembelea ubalozi wa Tanzania nchini humo sambamba na kutembelea makumbusho ya kimataifa ya mauaji ya Kimbali maarufu kama Rwanda Genocide Memorial ambapo waliona namna ya madhara makubwa ya maafa hayo nchini humo miaka ishirini iliyopita.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc imekua gumzo nchini humo huku vyombo vya habari vikiripoti kila aina ya tukio la klabu hiyo kiasi cha kuvutia mashabiki wengi nchini humo huku kitendo cha mkongwe wa klabu hiyo Haruna Niyonzima kuwa karibu na klabu hiyo kimewavutia wengi ambapo amekua kama balozi mzuri wa klabu hiyo nchini humo.
Jioni ya leo Agosti 14 kikosi hicho kimefanya mazoezi katika uwanja wa Amahoro nchini humo kujiandaa na mchezo huo wa kesho huku pia ikifanya ziara ya vyombo vya habari katika radio mbalimbali nchini humo.
Pia klabu hiyo imesafiri na baadhi ya mashabiki huku ikifungua tawi la klabu hiyo nchini humo ambapo sasa usajili wa mashabiki unaendelea pamoja na kupata kadi ya wanachama wa klabu hiyo.