Home Makala Yanga sc Yaibamiza Mafunzo

Yanga sc Yaibamiza Mafunzo

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mafunzo Fc katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Yanga sc iliiingia katika mchezo huo ikiwa na wachezaji wengi ambao hawatumiki mara kwa mara akiwemo Kipa Eric Johora,Paulo Godfrey huku mabeki wa kati wakicheza Ibrahim bacca na Yassin Mustapha pamoja na David Bryson aliyecheza upande wa kushoto huku Hertier Makambo na Balama Mapinduzi wakiongoza eneo la ushambuliaji.

Mafunzo walikua wa kwanza kupachika bao zuri dakika ya 9 likifungwa na Ahmed huku Yanga sc wakisawazisha kupitia kwa Balama Mapinduzi dakika ya 19 huku Hertier Makambo akifunga bao la pili dakika ya 52 bao ambalo lilisawazishwa na Abdulhakim dakika ya 55 kwa faulo iliyopatikana kutokana na uzembe wa beki Yassin Mustapha huku Msumari wa tatu kwa Yanga sc ukifungwa na Fiston Kalala Mayele kwa penati baada ya Yanick Bangala kufanyiwa faulo.

banner

Yanga sc imeendelea kujiandaa na michezo migumu inayofuata ya ligi kuu dhidi ya Azam Fc na Simba sc ambayo itaamua hatma ya ubingwa msimu huu huku pia wakikabiliwa na mchezo dhidi ya Geita Gold Fc wa kombe la shirikisho.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited