Home Makala Yanga sc Yaikalisha Tp Mazembe

Yanga sc Yaikalisha Tp Mazembe

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Tp Mazembe katika mchezo maarufu uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam na kurejesha matumaini ya timu hiyo kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Ikianza bila mastaa wake Feisal Salum na Stephane Aziz Ki Yanga sc ilipata bao la kwanza dakika ya saba ya mchezo baada ya kuunganisha krosi ya Djuma Shabani na mpira kumkuta mfungaji.

Mudathiri Yahya licha ya kuchezeshwa kama namba kumi alifanikiwa kuipatia Yanga sc bao la pili dakika ya 11 ya mchezo huku Tuisila Kisinda amerejesha kile wananchi wanakitaka kutoka kwake baada ya kuipatia klabu yake bao la tatu dakika ya 90+2.

banner

Yanga sc licha ya kupata zawadi za mahela pia imefikisha alama tatu nyuma ya Us Monastry iliyoko kileleni mwa msimamo wa kundi D ambalo licha ya Yanga sc lina timu za Real Bamako,Monastry na Tp Mazembe.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited