Home Soka Yanga Sc Yainyuka Singida Black Stars

Yanga Sc Yainyuka Singida Black Stars

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuifunga Singida Black Stars kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa New Amaan complex Visiwani Zanzibar.

Mchezo huo uliokua unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini ambapo kocha Miguel Gamondi aliwashangaza wengi akimuanzisha Dennis Nkane katika nafasi ya beki wa kulia badala ya Kibwana Shomari kutokana na Yao Kouasi Attouhoula kuwa majeruhi.

Uwepo wa Pacome Zouzoua na Cletous Chama sambamba na Aziz Ki nyuma ya Prince Dube kuliwafanya Black Stars kubaki nyuma muda mwingi wakipiga mipira ya juu kwenda kwa Elvis Rupia na pia kocha Patrick Aussems akimuanzisha Israel Mwenda kama winga wa kulia ili kuwazuia Yanga sc.

banner

Pacome Zouzoua alipiga shuti kali dakika ya 67 lililomshinda kipa Metacha Mnata na moja kwa moja kujaa wavuni na kuwahakikishia wananchi alama tatu muhimu.

Katika mchezo huo takribani kadi za njano nane zilitoka kwa wachezaji wa timu zote mbili huku pia makocha wasaidizi Dennis Kitambi na Mussa Ndaw wa Yanga sc nao walipata kadi na jumla kuzifanya zifike kumi.

Yanga sc sasa wapo kileleni mwa msimamo wakiwa na alama 24 wakishinda michezo yote nane ya ligi kuu ya Nbc nchini huku Singida Black Stars wakisalia nafasi ya pili na alama 22 wakicheza michezo takribani 9.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited