Home Makala Yanga Sc Yaisambaratisha Kurugenzi

Yanga Sc Yaisambaratisha Kurugenzi

by Sports Leo
0 comments

Ni muendelezo wa vipigo kwa timu za madaraja ya chini katika michuano ya kombe la shirikisho nchini ambapo Yanga sc ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Kurugenzi Fc katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kinda Clement Mzize alifanikiwa kufunga mabao manne dakika za 1′, 8′, 41, 45 katika mchezo huo huku Yussuph Athuman akifunga mabao mawili na Bryson Rafael akifunga moja huku beki wa kurugenzi akijifunga bao moja.

Yanga sc sasa imefanikiwa kufuzu hatua ya 32 bora ya michuano hiyo huku kocha Cedrick Kaze akiwaweka benchi mastaa kama Feisal Salum,Fiston Mayele,Jesus Moloko na Yannick Bangala pamoja na Khalid Aucho na kuwaanzisha Mzize,Aziz Ki,Morrison,Mauya na wengineo akiwemo majeruhi Djuma Shabani.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited