Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la shirikisho nchini baada ya kuifunga timu ya Ken Gold bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Uhuru.
Bao pekee la Fiston AbdulRazaq 42′ lilitosha kuwavusha Yanga sc hatua inayofuata baada ya kupata penati aliyoifunga kwa ustadi mkubwa kufuatia beki wa Ken Gold kuunawa mpira ndani ya boksi.
Licha ya ushindi huo mwembamba Yanga sc ilikosa magoli mengi kutokana na kushindwa kujipanga vizuri eneo la ushmabuliaji huku staa Carlos Carlinhos akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 82 baada ya kumpiga ngumi mlinzi wa Kengold.