Taarifa za ndani zinadai kuwa klabu ya Yanga sc inaweza kubadilishana wachezaji Jesus Moloko na Mbrazil Dario Federico da Silva anayeichezea Singida Big Stars ambayo imepanda kushiriki ligi kuu nchini.
Mabosi wa klabu ya Yanga sc wamefanikiwa kumuona Dario mara mbili wakati akiichezea klabu hiyo katika michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Zanaco Fc ya Zambia na dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo wamevutiwa na uwezo wake hivyo wanataka ajiunge kikosini mara moja huku wakiwapa Singida Big Stars mchezaji Jesus Moloko na kiasi cha pesa.
Bosi mkubwa kabisa wa Singida United ni mshabiki mkubwa wa klabu ya Yanga sc na ameshafanya hivyo kwa kuwapa Yanga sc mchezaji Feisal Salum na Ally Mtoni Sonso licha ya kuwa Feisal tayari alikua amesajiliwa na Singida United wakati huo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Taarifa ya mitandao ya kijamii ya Singida Big Stars imekanusha kuwepo kwa dili hilo lakini inasemekana hiyo ni geresha kwani tayari mazungumzo yamefikia mbali katika dili hilo na linaweza kukamilika muda wowote.