Baada ya kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika ya Kusini klabu ya Yanga sc imekabidhiwa fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 20 na Serikali ikiwa ni zawadi kutoka kwa Mh.Samia Suluhu Hassan.
Rais Samia ana utaratibu wa kununua kila goli kwa shilingi milioni kumi kwa hatua ya nusu fainali ambapo awalia alikua anatoa milioni tano kwa kila goli ambapo Yanga sc imefanikiwa kuvuna kiasi hicho cha pesa ikiwa na lengo la Mh Rais kuziongezea hamasa klabu katika michuano ya kimataifa.
Fedha hizo zimekabidhiwa jana uwanjani hapo na Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Balozi Dk.Pindi Chana ambapo zilipokelewa na nahodha wa klabu ya Yanga sc Bakari Mwamnyeto aliyeambatana na Rais wa klabu ya Yanga sc Eng.Hersi Said na mfadhili wa klabu hiyo Ghalib Said Mohamed maarufu kama Gsm.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc ni timu pekee iliyobaki katika michuano ya kimataifa msimu huu ambapo sasa itakwenda Afrika ya kusini ikiwa na lengo la kulinda ushindi huo ili kufuzu hatua ya fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.