Klabu ya Yanga imethibitisha kumsajili Kiungo wa CS Sfaxien ya Tunisia, Moussa Balla Conte (21) raia wa Guinnea kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kumalizana na klabu yake na kupewa ruhusa ya kukamilisha mazungumzo hayo na alfajiri ya leo ametua nchini na kusaini mkataba.
Nyota huyo raia wa Guinea ambaye pia alikuwa akiwaniwa na wekundu wa Msimbazi, Simba SC ametua mitaa ya Twiga na Jangwani kwa dau la USD 250,000 zaidi ya milioni 651 za kitanzania nje na fedha ya usajili ambayo klabu yake imechukua kama gharama ya kumnunu mchezaji huyo.
Tayari staa huyo ametambulishwa mchana wa leo kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na kuzua furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo kwani taarifa za awali zilisema kuwa mchezaji huyo aliichagua Simba sc licha ya Yanga sc kukamilisha malipo kwa klabu yake hiyo.
Usajili kwa Balla Conte ambaye anaenda kuchukua nafasi ya Khalid Aucho aliyepata ofa nono nchini Vietnam ni muendelezo wa utawala wa Yanga c katika ligi kuu ya soka nchini hasa upande wa soko la usajili ambapo mastaa mbalimbali kwa miaka ya hivi karibuni wamekua wakivutiwa zaidi kujiunga na timu hiyo.
Usajili huu ni matusi kwa Simba Sc ambapo inasemekana kuwa kocha Fadlu Davis alikua anamhitaji kiungo huyo na amefanya mazungumzo naye mara kadhaa kuhusu kujiunga na klabu hiyo ambapo inaonekana mabosi wa klabu hiyo ya Simba sc wamekua wazito katika kugombea wachezaji wazuri sokoni.