Home Soka Yanga Sc Yamtambulisha Mwamnyeto

Yanga Sc Yamtambulisha Mwamnyeto

by Sports Leo
0 comments

Baada ya tetesi za muda mrefu klabu ya Yanga sc imethibitishwa kumuongezea Mkataba nahodha wake Bakari Mwamnyeto ambapo sasa atasalia klabuni hapo kwa miaka miwili zaidi mpaka mwaka 2026 baada ya kusaini miaka miwili.

Mwamnyeto alikua akinyatiwa kwa ukaribu na Simba Sc lakini mchezaji mwenyewe aliamua kusalia Jangwani ambapo amekua akibadilishana nafasi kwa ukaribu na Ibrahim Bacca sambamba na Dickson Job ambao wamekua wakianza mara kwa mara.

Yanga sc ilimsajili Mwamnyeto msimu wa 2020/2021 akitokea Coastal Union ambapo alipofika alikabidhiwa kitambaa cha unahodha na amekua akiingoza timu hiyo mpaka kunyanya mataji matatu ya ligi kuu mfululizo huku akifanikiwa kuchukua pia kombe la Shirikisho sambamba na kufika fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (Caf).

banner

Katika mkataba huo Yanga sc imetumia Takribani milioni mia tatu kwa ajili ya malipo ya kusainia mkataba huo huku ikikubali kumpa mshahara wa milioni 15 za kitanzania kwa kila mwezi katika kipindi cha miezi miwili.

Ilikua ni ngumu kwa Yanga sc kuachana na nahodha huyo kutokana na ukweli kwamba ni ngumu kupata mbadala wake katika kipindi hiki hasa kwa wachezaji wazawa ambao wengi hawana ubora stahiki.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited