Kikosi cha wachezaji wa Yanga pamoja na viongozi kimeanza safari ya kuelekea nchini Algeria alfajiri ya leo kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya CR Belouizdad utakaofanyika siku ya Novemba 24 nchini humo.
Kikosi hicho ambacho kimesafiri asubuhi ya leo kimejumuisha mastaa wale ambao hawapo katika timu za taifa huku wengine wenye majukumu ya mechi ya kimatifa na timu za taifa wanarajiwa kuungana na kikosi siku moja kabla ya mchezo.
Mastaa kama Stephane Aziz Ki,Djigui Diarra na Khalid Aucho wenyewe wataunganisha ndege juu kwa juu huku wale walioko na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania wakitarajiwa kuondoka mapema kesho baada ya mchezo wa leo usiku baina ya Tanzania na Morocco.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Max Nzengeli,Pacome Zouzou,Jonas Mkude ni moja ya mastaa walionekana katika msafara wa klabu hiyo kuelekea nchini Algeria tayari kuzisaka alama tatu za hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.