Home Makala Yanga sc Yapewa Wasudan Caf

Yanga sc Yapewa Wasudan Caf

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga ya Tanzania imepangwa kuanza na timu ya Zalan ya Sudan Kusini katika hatua ya awali ya kombe la klabu bingwa barani Afrika kwa mujibu wa droo iliyofanyika hivi sasa nchini Misri.

Yanga sc imefanikiwa kuingia katika droo hiyo baada ya kuwa mabingwa wa ligi kuu nchini ambapo pia mshindi kati yao atakutana na mshindi kati ya St. George ya Ethiopia au Al Hilal ya huko huko Sudan ambayo sasa inanolewa na kocha Frolent Ibenge.

Zalan Fc ni Mabingwa wa ligi kuu ya Sudan Kusini mwaka 2018 ikitokea mji wa Rumbek ambapo Yanga sc watakua na kazi ya kupambana ili kuwafunga ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele hata wakifunga na mshindi kati ya Al ahly Tripoli ya Libya na St.George ya Ethiopia.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited