Home Makala Yanga Sc Yarejea Kileleni

Yanga Sc Yarejea Kileleni

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kurejea katika kilele cha ligi kuu nchini baada ya kuibuka na alama tatu katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam majira ya saa moja usiku.

Ikiingia uwanjani bila kocha mkuu wake Nasreddine Nabi ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi kuu pamoja na  mshambuliaji kiongozi Fiston Mayele mwenye majeraha timu hiyo ilishindwa kuifungua safu ya ulinzi ya klabu ya Prisons ambao waliamua kupaki basi muda mwingi wa mchezo huo.

Licha ya kufanya mabadiliko mara kadhaa ikiwaingiza Farid Musa,Djuma Shabani na Benard Morrison Yanga sc ililazimika kusubiri mpaka dakika ya 89 ya mchezo ambapo Feisal Salum aligongeana vizuri na Farid Musa na kuandika bao pekee katika mchezo huo ambalo lilibeba matumaini ya mashabiki wengi wa klabu hiyo ambao bado wanasherehekea kucheza michezo 49 ya ligi kuu bila kupoteza.

banner

Yanga sc sasa imefikisha alama 35 za ligi kuu ikicheza michezo 14 na kukaa kileleni huku Simba sc ikiwa nafasi ya pili na alama 34 katika michezo 15 na Azam Fc ipo nafasi ya tatu na alama 32 ikicheza michezo 14.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited