Klabu ya Yanga sc imemtambulisha benchi jipya la ufundi litakalokuwa chini ya kocha Roman Folz baada ya kocha huyo kuamua kuja na wasaidizi wake na kuwaondoa wale waliokua wamejiariwa katika nafasi hizo tangu mwanzo.
Kocha huyo mwenye miaka 35 ameamua kuja na Mkurugenzi wake wa Ufundi ambaye ndiye atakua anasimamia Dira ya kiufundi ya klabu hiyo akichukua nafasi ya Abdulhamid Moalin ambaye sasa ameondoka kwenda Cr Belouizdad kuungana na aliyekua kocha wa Yanga sc Sead Ramovic.
Yanga sc imemtambulisha Paul Matthews ambaye ataungana na Roman Folz katika nafasi hiyo adhimu kabisa klabuni hapo.
Mbali na Matthew pia klabu hiyo imemtambulisha rasmi kocha msaidizi Manu Rodriguez ambaye yeye atakua na kazi ya kumsaidia kocha mkuu katika utekelezaji wa mipango ya timu ndani ya uwanja ambapo ana umri wa miaka 33 tu mpaka sasa akiwa amewahi kufanya kazi maalumu ya kuwanoa washambuliaji katika nchi za ulaya na America Kusini.
Pia Yanga sc imemtambulisha kocha wa viungo raia wa Afrika kusini Tshephang Mokaila ambaye atakua na kazi ya kuhakikisha utimamu wa mwili wa wachezaji hao.
Wadau wengi wa soka nchini wameonyesha kuvutiwa na utimamu wa mwili wa kocha huyo ambaye pia ni mtaalamu wa kupiga karate.
Yanga sc imebadilisha benchi lote la ufundi baada ya kuachana na kocha Miloud Hamdi ambaye ameelekea Ismailia ya nchini Misri ambapo sasa benchi lina kazi kubwa ya kuendeleza historia ya mataji klabu hapo ambapo msimu ulioisha imebeba mataji matano ya ndani na nje ya nchi.