Home Makala Yanga Yachakazwa Na Kagera Sugar 3-0

Yanga Yachakazwa Na Kagera Sugar 3-0

by Sports Leo
0 comments

Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime imewalamba Yanga mabao 3-0 kwenye mchezo wa ligi kuu bara uliochezwa leo Januari 15 uwanja wa Uhuru.

Yusuph Mhilu amekuwa wa kwanza katika kulifungua goli la Kagera Sugar kwa kupiga mpira wenye kasi uliomshinda mlinda mlango wa Yanga Faruku Shekhalo dakika ya 13.

Bao la pili lilifungwa na Ally Ramadhani dakika ya 66 katika kipindi cha pili cha mchezo huku dakika ya 89 Peter Mwalanzi alimalizia goli la tatu alililofunga kwa kichwa.

banner

Yanga ambao kwa sasa wapo chini ya Mbelgiji Luc Eymael wamejikuta mchezaji wao Mo Banka akipewa kadi nyekundu dakika ya 44 baada ya kuwachezea rafu wachezaji wawili wa Kagera Sugar Adala Siseme dakika ya 26 na Kelvin Sabato dakika ya 44.

Kagera Sugar imekuwa nafasi ya nne inafikisha pointi 27 katika mechi ya 17 huku Yanga ikiwa nafasi ya nane ikiwa na pointi 25 mechi ya 13.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited