Home Makala Yanga Yapigwa Bao Dodoma Fc

Yanga Yapigwa Bao Dodoma Fc

by Sports Leo
0 comments

Dodoma Fc imefanikiwa kunasa saini ya kiungo aliyekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga kwa mda mrefu,Cleofas Mkandala kutoka TanzaniaPrisons.

Afisa habari wa Dodoma Fc,Ramadhani Juma amesema kuwa baada ya dirisha kubwa la usajili kufunguliwa,timu imeendesha zoezi hilo kwa mujibu wa mapendekezo ya benchi la ufundi na wengine waliokwisha kusajiliwa ni Michael Chinedu kutoka Alliance na Seif Karie kutoka Lipuli Fc.

Dodoma Fc imewaongezea mikataba wachezaji wao 11 wakiwa ni Emmanuel Mseja,Hussein Msalanga,Anderson Solomoni,Hassan Kapona,Mbwana Kibacha,Rajabu Seif ,Steven Mganga,Jamal Mtegeta,Deusdelius Kigawa,Santos Thomas na Khamis Mcha.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited