Home Makala Yanga,Molinga Ndoa Yaelekea Ukingoni

Yanga,Molinga Ndoa Yaelekea Ukingoni

by Sports Leo
0 comments

Sasa ni rasmi Uongozi wa klabu ya Yanga utaachana na Strika wao Mkongomani  David Molinga Falcao na nafasi yake kuchuKuliwa na Strika kutoka Tp Mazembe Owe Bonganya baada ya uongozi kufikia makubaliano ya kuvunja Mkataba na Striker huyo.

Chanzo cha ndani kinaeleza kuwa Molinga anaachwa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha hasa katika Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Biashara Utd.

Molinga baada ya kutolewa alisusa na kuondoka akiwa kavaa nguo za kawaida baada ya kuvua jezi za Yanga .

Hiyo na nyingine ni Miongoni mwa sababu zinazofanya Staa huyo kuachwa na Yanga kwa tafsiri kuwa ana kiburi na alionesha dharau kwa kocha na uongozi wa Yanga.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited