Kocha wa zamani wa Yanga sc Mwinyi Zahera ametoa ufafanuzi juu taarifa zilizosambaa juu ya kuitwa kwa kiungo wa klabu ya Yanga sc Mukoko Tonombe katika kikosi cha timu ya Taifa ya Congo Drc.
“Tonombe Mukoko yupo ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Congo cha wachezaji 45 ambao wameorodheshwa mwezi mmoja kabla ya michezo”Alisema Zahera
Alitumiwa barua ya kujulishwa kwamba yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kuitwa kwenye kikosi,lakini pia inawezekana asiitwe pia kama hali ya Covid_19 kama itakuwashida (namna ya kuingia Congo DR)
Ijumaa hii tutaita wachezaji rasmi,Zamani tulikua tunaita wachezaji 23 wa mwisho, lakini Kutokana na Covid-19, tutataja wachezaji 33.
Hivyo Tonombe Mukoko ameorodheshwa katika majina yale 45, lakini bado hajaitwa katika orodha ya mwisho, inawezekana aitwe au asiitwe.