Home Makala Zahera Kuti Kavu Coastal Union

Zahera Kuti Kavu Coastal Union

by Sports Leo
0 comments

Taarifa kutoka ndani ya Uongozi wa klab ya Coastal Union ni kwamba uongozi wa klabu hiyo umefikia makubaliano rasmi ya kusitisha mkataba na kocha wao mkuu raia wa Congo DRC, Mwinyi Zahera baada ya kutoridhishwa na kiwango cha Timu hiyo tangu akabidhiwe majukumu ya kukionoa.

Zahera alijiunga na Coastal Union msimu huu lakini mpaka sasa kikosi cha timu hiyo kimeshindwa kupata ushindi katika michezo yake yote ya ligi kuu nchini ambapo katika michezo mitano kimepata sare mbili na kufungwa michezo mitatu.

Inasemekana tayari makubaliano yalishafikiwa baina ya timu hiyo na kocha huyo na sasa kilichobaki ni kutangaza tu huku akiwa mpaka sasa hayuko na timu ambayo imeelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo dhidi ya Ihefu Fc.

banner

Zahera amekua na wakati mgumu kufundisha soka nchini tangu aachane na Yanga sc ambapo alijiunga na Polisi Tanzania ambapo hakudumu na sasa Coastal Union napo ameshindwa kuipa mafanikio.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited