Kutokana na usajili wa nguvu uliofanyika Jangwani kocha Mwinyi Zahera ameanza kupata mtihani wa kupanga wachezaji baada ya wengi kuonekana kupania kuingia kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Golini kiwango kilichooneshwa na kipa Metacha Mnata katika mechi dhidi ya Township Rollers ambapo kipa huyo alidaka penati kimemfanya kocha huyo kupata wakati mgumu wa kuamua nani aanze katika mechi ya ufunguzi leo dhidi ya Ruvu shooting ambapo umahiri wa kipa namba moja Farouk shikalo unajulikana na kufanya kocha Zahera aumize kichwa.
Upande wa mabeki pacha ya Yondani na Lamine inaonekana kukubalika japo pia uwepo wa Ally Mtoni na Mustapha Selemani unafanya kocha huyo kupasua kichwa japo kwa upande wa mabeki wa pembeni kuna unafuu kutokana na majeruhi ya Paulo Godfrey na Ally Ally.
Safu ya viungo imeshikwa na Mohamed Issa na Papy Tshitshimbi huku Mapinduzi Balama na Patrick Sibomana wakitokea pembeni japo majeruhi ya Mohamed Issa yatampa nafasi ya kuamua kati ya Feisal Salum na Abdulazizi Makame.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Nafasi ya ushambuliaji Juma Balinya na Sidney Urikhob wana nafasi ya uhakika mbele ya Issa Bigirimana japo uwepo wa David Molinga unatishia uhai wa pacha hiyo.