Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Azam Fc Yahaya Zayd amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia katika klabu hiyo kwa miaka miwili mingine mpaka mwaka 2026.
Zayd ambaye amelelewa katika akademi ya klabu hiyo mkataba wake wa sasa ulikua unamalizika mwishoni mwa msimu huu na hivyo kusaini mkataba huo mpya kunazima majaribio ya klabu zingine kumchukua staa huyo.
Usajili huo ni pendekezo la mwalimu wa klabu hiyo Yousouph Dabo ambaye anahitaji kuendelea na kiungo huyo mshambuliaji katika mipango yake klabuni humo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pamoja na kusaini mkataba mpya kiungo huyo ana kazi nzito ya kufanya ili kuweza kumshawishi kocha Dabo awe anamuanzisha mara kwa mara kikosini ambapo kwa sasa eneo la namba kumi limeshikwa na Feisal Salum huku winga akipambania namba na Ayoub Lyanga,Idd Nado na Kipre Junior pamoja na Gibri Sillah ambaye huwa anaanza mara kwa mara.