Home Soka Ajibu Atimuliwa Kambini

Ajibu Atimuliwa Kambini

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha Mkuu wa timu ya Simba sc Sven Vandebroekamemtimua kambini kiungo mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu kutokana na kosa la kuchelewa kambini.

Wachezaji wa Simba waliripoti kambini Mei 27 ambapo walipofika walifanyiwa vipimo asubuhi na kuanza kufanya mazoezi mepesi jioni kwenye uwanja wao wa Bunju.

Sven amesema kuwa Ajibu hakutoa taarifa jambo lililosababisha amsimamishe kwa muda atamrejesha kikosini pale atakapoona inafaa.

Ajibu ndani ya Simba amefunga bao moja na kutoa pasi nne za mabao aliibukia kikosini hapo akitokea Yanga msimu wa 2019/20 alipokua ameonyesha kiwango kikubwa.

Ajibu amekuwa na majanga ya kukosa namba kikosi cha kwanza kutokana na upana wa kikosi hivyo hili ni janga lingine anakutana nalo la kuchimbishwa kambini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited