Beki wa timu ya Kmc Ally Ally amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu ya Yanga sc leo hii jioni baada ya mkataba wake na timu ya Kmc kufikia tamati hivi karibuni.
Beki huyo mwenye asili ya visiwa vya Pemba mwenye mwili mdogo na akili nyingi ya kucheza mpira amesaini kandarasi hiyo ya miaka miwili jioni ya leo huku akilakiwa na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo waliompokea katika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani Kariakoo.
Kusaini kwa beki huyo kunamaliza tetesi za muda mrefu za beki huyo kuhusishwa na wanajangwani hao baada ya tetesi kusambaa kwa muda mrefu kuwa amemalizana na klabu hiyo ya Jangwani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ally Ally ni beki mzoefu wa ligi kuu ya Tanzania bara ambapo alijiunga na Kmc inayomilikiwa na manispaa ya Kinondoni baada ya kuwa ameitumikia Stand united ya Shinyanga.