Licha ya kuiongoza Napoli kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Genk na kufuzu hatua ya mtoano timu ya Napoli imemtimua kocha huyo saa moja baada ya mechi hiyo.
Kocha huyo mwenye miaka 60 ametimuliwa baada ya mechi hiyo kufuatia kutokua na mwenendo mzuri kwenye ligi akipata ushindi mara moja kwenye mechi kumi na kuiweka timu hiyo nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Italia (Serie A).
Inasemekana Napoli inaweza kumuajiri Gennaro Gattuso kuchukua nafasi hiyo ya Carlo Ancelloti huku wadau wa michezo wakimhusisha na kurudi ligi ya Uingereza miaka nane tangu atimuliwe na Chelsea licha ya kuipa kombe.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.