Kampuni ya Azam Tv imeingia mkataba na bodi ya ligi kuu Tanzania bara pamoja na Shirikisho la soka nchini Tff kudhamini matangazo ya Televisheni kwa muda wa miaka 10 kwa kiasi cha shilingi Biloni 225.
Katika mkataba huo klabu za ligi kuu zitakua na malipo makubwa kila mwezi ambapo kila timu itapata mgao wa kiasi cha milioni 40 kwa ajili ya kulipa mishahara ya wachezaji huku bingwa wa ligi kuu atapata Bonasi ya milioni mia tano na mshindi wa pili akipata milioni 250 na wa tatu milioni 225 huku zawadi zikiendelea mpaka mshindi wa sita.