Home Soka Baleke Atua Libya

Baleke Atua Libya

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya TP Mazembe imemtoa tena kwa mkopo mshambuliaji Jean Baleke kwenda kucheza katika klabu ya Al Ittihad ya nchini Libya baada ya kuachana na klabu ya Simba sc wakati wa usajili wa dirisha dogo msimu huu.

Baleke tayari amemalizana na kuagwa Simba baada ya muda wake wa mkopo kuisha na sasa atakuwa akikiwasha katika klabu hiyo ya Libya kwa mkataba wa mwaka mmoja hadi Januari 30, 2025.

Awali taarifa zilidai kuwa staa huyo anarejea Tp Mazembe ambapo kocha wa klabu hiyo alikua akivutiwa na takwimu zake na kutaka kumrudisha klabuni hapo lakini taarifa hii ilitolewa mapema leo hii inamaliza utata kuhusu hatma ya mshambuliaji huyo hatari.

banner

Simba sc iliamua kuacha na Baleke ili kuziba nafasi hiyo kwa kumsajili mshambuliaji wa moja kwa moja badala ya mshambuliaji huyo wa mkopo huku kanuni ya kuwa na wachezaji 12 wa kigeni ikiwabana na kuwalazimisha kuachana na staa huyo aliyefunga mabao 8 katika ligi kuu nchini msimu huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited