Licha ya kusajiliwa kwa mbwembe na majigambo mengi kwa wanajangwana mpaka sasa Issa Bigirimana hajaonyesha kile ambacho wanayanga wengi walikitarajia kutoka kwake licha ya kuwahi kuungana na timu mkoani Morogoro katika kambi ya maandalizi ya msimu.
Iko hivi,Sportsleo imebaini sababu kubwa ya staa huyo wa Burundi kutocheza mpaka sasa ni majeraha ya nyama za paja yanayomsumbua kwa muda mrefu tangu akiwa kambini mkoani Morogoro na amekua akipata nafuu japo hajapona kabisa.
Majeraha hayo yamemfanya kiungo mshambuliaji huyo kutoungana na timu mkoani Mwanza katika kambi maalumu ya kujiandaa na mechi ya kimataifa dhidi ya Zesco ya Zambia.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Sportsleo ilifanikiwa kumuona kiungo huyo uwanja wa taifa siku ya mchezo wa Taifa stars dhidi ya Burundi mchezo ambao Taifa stars iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwa penati na baada ya kufatilia kwa undani ndipo lilipobaini taarifa hiyo.