Klabu ya Simba sc imemtambulisha rasmi Ofisa mtendaji mkuu mpya ambaye atachukua nafsi ya Crecentious Magori ambaye mkataba wake wa miezi sita umeisha.
Bosi huyo mpya wa timu hiyo aliyetambulishwa mbele ya waandishi wa habari anaitwa Senzo Masingisi raia wa Afrika Kusini ambaye ataiongoza klabu hiyo kama Afisa mtendaji mkuu baada ya Magori kuivusha katika kipindi cha mpito.
Masingizi ana uzoefu wa uongozi wa soka baada ya kuwa mjumbe katika shirikisho la soka la Afrika kusini huku akiwa kushika nafasi za uongozi katika vilabu vya Orlando Pirates na Fc platnum.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.