Home Soka Boxer Ajiunga Singida Big Stars

Boxer Ajiunga Singida Big Stars

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Singida Big Stars imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa kulia Paul Godfrey Boxer Kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kuisha.

Beki huyo ambaye alipandishwa katika timu kubwa ya Yanga sc akitokea timu ya vijana na kocha Mwinyi Zahera amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga sc chini ya kocha Nasredine Nabi ambaye humtumia Kibwana Shomari zaidi na Djuma Shabani katika eneo la mlinzi wa kulia huku ikielezwa kuwa klabu ya Yanga sc haikua na mpango wa kumuongezea mkataba mpya.

Singida Big Stars imekua kimbilio la wachezaji wengi wa klabu kubwa nchini baada ya mikataba yao kumalizika wakiwa hawana uhakika wa kuongezewa mikataba mipya na mpaka sasa imehusishwa na mastaa kibao japo tayari imekamilisha usajili wa Aziz Andambwile na Habib Kyombo kutoka Mbeya kwanza Fc.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited