Mambo yamezidi kumnyookea beki wa Yanga sc Paulo Godfrey “Boxer” baada ya jana kuvaa jezi ya timu ya taifa kwa mara ya kwanza huku pia ikidaiwa timu hiyo imemuongezea mshahara baada ya kuonyesha kiwango bora.
Beki huyo aliyekuwa akiitumikia timu ya vijana ya timu hiyo(Yanga B) alipandishwa na kocha Mwinyi Zahera baada ya timu hiyo kushindwana na beki Hassan Kessy aliyetimkia Nkana Red Devil ya Zambia hivyo kuwalazimisha wanajangwani hao kumpandisha beki huyo ili kuwa mbadala wa Juma Abdul anayesumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Neema ilizidi kumshukia kinda huyo baada ya kufanya vizuri katika mechi ya watani wa jadi akimdhibiti vilivyo winga Shiza Kichuya na Emmanuel Okwi na kufanya aaminiwe zaidi na kumpoka namba Juma Abdul.
Beki huyo aliyebadilishwa nafasi kutoka winga ameongezewa mshahara kutoka laki nne za kitanzania mpaka milioni moja na nusu kwa mwezi ili kuendana na thamani yake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga imeweka kambi mjini Morogoro huku baadhi ya wachezaji wakiwa kambini na timu ya taifa ambayo jana ilitoa suluhu na Kenya katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan).