Makinda wa Yanga Paulo Godfreyc”boxer” na Balama Mapinduzi wapo kwenye hatihati ya kuukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco united ya Zambia baada ya kukumbwa na majeraha.
Boxer aliumia katika mechi ya kirafiki jijini Arusha na mpaka leo bado hajapona akiwa tayari kashakosa mechi ya ligi dhidi ya Ruvu shooting huku akikosa mechi ya awali dhidi ya Zesco na kuna uwezekana mkubwa wa kuukosa mchezo wa marudiano huku kwa upande wa Balama yeye akiendelea kuuguza majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya Zesco ambapo alicheza nafasi ya beki wa pembeni kuziba pengo la Boxer.
Hata kukosekana kwa wachezaji hao hakuwezi kumpasua kichwa kocha Mwinyi Zahera kutokana na kurejea kwa Juma Abdul huku pia Ally Ally akiwa tayari kucheza nafasi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga italazimika kushinda mchezo huo ama kutoa sare ya kuanzia mabao 2 na kuendelea ili kupata nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.