Home Soka Breaking News..Kiungo Simba Atimkia Kaizer Chief

Breaking News..Kiungo Simba Atimkia Kaizer Chief

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa Simba sc James Kotei amejiunga na timu ya Kaizer Chief inayoshiriki ligi kuu ya Afrika ya Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya klabu hiyo kutoa taarifa rasmi katika mtandao wa kumalizana na kiungo huyo.

Kotei mwenye miaka 25 ameondoka Simba akiwa amewasaidia kutwaa mataji ya ligi kuu mara mbili mfululizo na kuwawezesha kufika katika hatua ya robo fainali katika ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ambayo walitolewa na Tp Mazembe huku Kiungo huyu Mghana akicheza karibuni mechi nyingi za ligi kuu na ligi ya mabingwa Afrika.

banner

Kiungo huyo makini hasa wa ulinzi anaondoka klabuni hapo kufuatia uongozi wa klabu hiyo kutompa mkataba mpya licha ya ule wa awali kumalizika huku kukiwa hakuna jitihada zozote za kumuongezea kama ilivyokua kwa mastaa wengine ambao wamepewa mikataba mipya.

Awali suala la kiungo lilizua sintofahamu huku ikidaiwa uongozi wa klabu hiyo umegawanyika pande mbili kuhusu kumpa ama kutompa mkataba mpya huku sehemu kubwa ya mashabiki wakitaka kiungo huo apewe mkataba mpya ili pia kuzima tetesi za kutakiwa na watani wao wa jadi Yanga sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited