Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amekiri kukosekana kwa kiungo Carlos Carlinhos, kwenye kikosi chake ni pengo kwa sababu tayari alikuwa ameshaanza kuchanganya na kufanya vema baada ya kuanza kucheza akitoka kwenye chumba cha majeruhi
Hata hivyo kocha huyo raia wa Burundi amesema amekiandaa kikosi chake kimbinu kumpa matokeo chanya kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union utakaopigwa keshokutwa Alhamisi katika uwanja wa Mkwakwani
Yanga inatarajia kucheza mechi yake ya Ligi Kuu Alhamisi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga dhidi ya Coastal Union na itamkosa Muangola huyo ambaye alilimwa kadi nyekundu Jumamosi wakati timu hiyo ikicheza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam dhidi ya Ken Gold ya Mbeya kwenye Kombe la FA.
Kaze alisema Carlinhos aliingia kirahisi kwenye mtego ambao alishinda kuutambua, hivyo kujikuta akifanya kosa ambalo hakulitarajia.
“Tukio halikuwa kubwa kivile, lakini mwenyewe alishindwa kujidhibiti na kujikuta akiingia kwenye mtego kirahisi. Ni pengo kwa timu kwa sababu kwenye mechi chache ambazo amecheza tangu atoke majeruhi, ameonyesha kuwa ana msaada mkubwa kwa wenzake,” alisema Kaze.
Mchezaji huyo ndiye aliyefunga bao pekee Februari 20 kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, akitokea benchi, ikiwa ni mechi yake ya kwanza, baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiwa majeruhi.
Hata hivyo, Kaze alisema anachoshukuru ameomba radhi na mambo yamekwisha, lakini wao wanakwenda kucheza mechi zinazofuata na wachezaji waliopo.
Kelekea mchezo dhidi ya Coastal Union, kaze amesema mpango mkubwa ni kupata matokeo chanya na tayari amefanyia kazi kasoro zilizojitokeza katika kikosi chake na sasa wachezaji wake wapo vizuri, hivyo anaamini atapata matokeo chanya na kuzidi kujiimarisha kileleni.
“Kwa sasa tunatazama namna gani tunaweza kupata matokeo chanya kwenye mechi zijazo, hilo ni la msingi kwetu, katika hilo ni kuendelea kuwapa mbinu washambuliaji ili kuweza kumalizia nafasi wanazotengeneza uwanjani,” alisema Kaze.
Alisema wamekuwa wakitengeneza nafasi zaidi ya tano na kushindwa kumalizia jambo ambalo amekuwa nalo makini kwa washambuliaji wake katika mazoezi.
“Kila kitu kitakuwa sawa mashabiki waendelee kutupa sapoti kwa kuwa ushindani.