Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc Senzo Mazingisa amesema atamshtaki makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela Baada kusema kuwa Yanga wameanza mazungumzo na nyota wa Klabu ya Simba Clatous Chama.
Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mazingisa ameshangazwa na Kauli hiyo na amesema atawashitaki TFF au FIFA.
Senzo amesisitiza Kama kiongozi huyo alikuwa anaongea kuwafurahisha mashabiki wake itamutokea puani kwa kuwa mchezaji huyo ni mali ya Simba na ana mkataba.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia Senzo ameshangaa kuona Kiongozi mkubwa wa Yanga akiongea kwenye media bila wasiwasi akijadai ameongea na Chama ni Kosa kubwa kutangaza kwenye vyombo vya habari umeongea na mchezaji ambaye ana mkataba na Klabu yake huo ni ushahidi tosha wa kumshitaki mtu/klabu kokote.