Kenya imethibitisha ubabe wake katika Kundi A la Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani yanayoendelea katika nchini za Tanzania,Kenya na Uganda maarufu kama (CHAN) PAMOJA 2024 baada ya kushinda kwa kishindo 1-0 dhidi ya Zambia katika mcheso uliofanyika katika uwanja wa Moi International Sports Centre, Kasarani Jumapili Agosti 17 2025.
Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua,Goli la ushindi lilifungwa na Ryan Ogam dakika ya 75 ya kipindi cha pili likiwaweka Harambee Stars kwenye nafasi ya kwanza ya kundi A la michuano hiyo wakiwa wamekusanya alama 10, huku Zambia ikiondoka katika mashindano bila alama yoyote.
Wakati huo huo, Morocco ilipiga DR Congo 3-1 katika mchezo mwingine, na hivyo kuifanya Kenya na Morocco kufuzu kwenye robo fainali, huku DR Congo ikabaki nafasi ya tatu na moja kwa moja kuaga mashindano hayo licha ya kuonyesha uwezo mkubwa
Kenya itabaki jijini Nairobi kukutana na Madagascar katika robo fainali ya Ijumaa, huku Morocco ikisafiri kukabiliana na Tanzania katika mchezo mwingine wa hatua hiyo.
Ryan Ogam kwa mara nyingine aliibuka staa wa mchezo huo ambao ulikuwa sawa hadi dakika ya 75, wakati mchezaji aliyeingia kutokea benchi Boniface Muchiri alipopata nafasi upande wa kulia na kutoa pasi nzuri ndani ya eneo la penalti na kumkuta Ogam ambaye aliudhibiti mpira vizuri kabla ya kumpita kwa utulivu Charles Kalumba wa Zambia, na kufurahisha mashabiki 27,000 waliojaza uwanja huko Nairobi.
Goli hilo lilikuwa tuzo ya uvumilivu wa muda mrefu wa Kenya baada ya kutawala mpira na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo zilizuiliwa au kukataliwa na Kalumba, ambaye alikuwa na usiku wa kuvutia licha ya kushindwa kwa timu yake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tayari wakiwa na uhakika wa nafasi ya robo fainali, Kenya iliingia kwenye mchezo huo kwa nia ya kuthibitisha uwezo wake kama moja kati ya wagombea wa ubingwa wenye nguvu wakitaka kumaliza wakiwa kileleni mwa kundi A.
“Wakati kila mtu aliposema tupo kwenye ‘Kundi la Kifo’, pengine tungekuwa hatuna alama yoyote baada ya michezo minne. Lakini tumefika kileleni, na sasa tunataka kufurahia maono kutoka hapo juu,” alisema kocha Ben McCarthy alisema kabla ya mchezo kuanza.
Kenya tayari ilikuwa imeshinda Morocco na DR Congo mapema katika kundi hilo, matokeo yaliyowafanya wegi kuwa na mshangao wa mashindano hayo kwa kuwa hawakutegemea kama ingeweza kushinda michezo hiyo.
Dhidi ya Zambia, walionyesha ukomavu wa kimkakati na uthabiti wa kusaidia kufanikisha ushindi wa tatu katika michezo minne, wakimaliza kwa alama 10 na goli moja tu lililofungwa dhidi yao katika awamu ya makundi.