Timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Angola katika mchezo wa pili wa kundi C wa Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN), na sasa itakabiliana na Morocco katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo ambao utamaliza utata wa timu itakayofanikiwa kufuzu robo fainali ya michuano hiyo.
Mabao ya DR Congo yalifungwa na Jephte Kitambala katika dakika ya 58 kwa kichwa akiunganisha mpira wa faulo uliopigwa kiufundi na winga Basiala Agee huku mabeki wa Angola wakibaki na mshangao wasijue la kufanya na bao la pili lilifungwa na Jonathan Mokonzi Katumbwe katika dakika ya 70, huku Angola ikionyesha uwezo mdogo wa kushambulia.
Matokeo haya yanaiweka DR Congo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kupata alama tatu, sawa na Morocco ambayo pia ina alama tatu baada ya mchezo wao wa kwanza. Hii inamaanisha mchezo wao ujao utakuwa wa kuamua nani atafuzu hatua ya robo fainali kwani timu hizo zote zina alama sita kila mmoja zikiwa zimecheza michezo mitatu mitatu.
“Tulicheza kwa nidhamu na kufuata mipango yetu,” alisema kocha wa DR Congo, Otis Ngoma. “Sasa tunajiandaa kwa Morocco kwa kujua kuwa ni mchezo mgumu.”Alimalizia kusema kocha huyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kwa upande wake, Angola ambayo tayari imepoteza michezo miwili, imeondolewa kwenye mashindano hata kabla ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya Zambia ambapo italazimika kucheza ili kukamilisha ratiba tu.
Michezo ya mwisho ya kundi A inatarajiwa kuchezwa siku ya jumapili Agosti 17 ambapo Kenya itavaana na Zambia ili kutafuta nafasi ya kufuzu robo fainali huku kimbembe kikubwa kikiwa mchezo baina ya Congo DR dhidi ya Morroco ambao unatarajiwa kuwa mkali kwani atakayeshinda ndio atafuzu hatua ya robo fainali kutokea kundi hilo la A.
Michuano ya Chan kwa mwaka 2025 inafanyika katika nchi tatu za Tanzania,Kenya na Uganda ambapo pia nchi hizo ndio zitatumika kuandaa michuano ya Afcon kwa mwaka 2027.