Home SokaChan 2025 Uganda Cranes Yafuzu Robo Fainali Chan

Uganda Cranes Yafuzu Robo Fainali Chan

by Dennis Msotwa
0 comments

Timu ya soka ya Taifa la Uganda maarufu kama Uganda Cranes imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) baada ya kulazimisha sare ya 3-3 dhidi ya Afrika kusini katika mchezo huo uliokua mkali na wa kusisimu uliofanyika siku ya Jumatatu Agosti 18 2025.

Ukizungumzia kupambana mpaka dakika ya mwisho ndio kiliochafanya na timu hiyo ambapo Uganda ilithibitisha hilo wakati walipopambana kutoka kwenye ushindi wa 3-1 wa Afrika Kusini kwnda kwenye sare ya 3-3 na kufuzu kwa robo fainali ya mashindano ya TotalEnergies CAF African Nations Championship (CHAN) 2024 yanayoendelea katika nchi za Tanzania,Kenya na Uganda.

Uganda Cranes Yafuzu Robo Fainali Chan-sportsleo.co.tz

Kufikia mechi hiyo muhimu ya kundi C usiku wa Jumatatu, Uganda ilihitaji pointi moja tu, wakati Bafana Bafana walihitaji ushindi kamili kwenye uwanja wa Nelson Mandela, Namboole ili kufuzu hatua hiyo muhimu.

Baada ya mashambulio kadhaa kwenye goli la Afrika Kusini, Uganda iliongoza kwa bao la Jude Ssemugabi baada ya dakika 31 lakini Katika nusu ya pili, Bafana Bafana walijitokeza kwa nguvu na kufunga bao la kusawazisha kupitia Ramahlwe Mpahahlele baada ya dakika 52. Mlinzi wa Uganda Joel Mutakubwa alikuwa amepiga mpira ndani ya uwanja, na Mpahahlele akamalizia kwenye goli.

Awali, mwamuzi alikuwa amebatilisha bao hilo, lakini maofisa wa VAR walikubali kuwa lilikuwa sahihi na kuzidi kuleta presha kwenye mchezo huo hasa upande wa mashabiki.

Timu ya Afrika Kusini ilidhibiti mchezo huku wakishambulia kwa wingi na dakika sita baadaye, Thabiso Kutumela alifunga bao la pili kwa wageni na kuifanya 2-1 huku Uganda Cranes walijaribu kupambana kwa kufanya mabadiliko, lakini timu ya Afrika Kusini iliendelea kushambulia kwa kasi ya ajabu.

Baada ya makosa ya mlinzi wa Uganda, Ndabayithethwa Ndlondlo alifunga bao la tatu kwa Bafana Bafana kwa chipu nzuri iliyotulia kwenye kona ya goli na kuifanya matokeo kuwa  3-1.

Lakini mchezo ulibadilika ghafla wakati wenyeji Uganda walipopatiwa penalti baada ya dakika 88 wakati mlinzi wa Afrika Kusini Keagan Johannes alipomwangusha mchezaji wa Uganda ndani ya boksi na mshambuliaji tegemeo Allan Okello alisimama na kufunga penalti na kuifanya 2-3.

Katika dakika ya sita ya nyongeza, Uganda ilipata penalti ya pili baada ya mpira kuguswa na mkono ndani ya boksi na nahodha Rogers Torach alifunga penalti hiyo na kuifanya 3-3 na kuifanya siku hiyo kuwa sherehe mara tu baada ya filimbi ya mwisho.

Sare hiyo ya Uganda, pamoja na sare katika mechi nyingine ya Kikundi C kati ya Algeria na Niger iliyochezwa Nairobi, inamaanisha kuwa Uganda imemaliza kwenye nafasi ya kwanza ya kundi hilo kwa pointi 7 na kufuzu kwa robo fainali.

Hii ni mara ya kwanza Uganda Cranes wanafuzu kwenye hatua ya knockout katika mashindano ya CHAN katika historia ya Taifa hilo kwa upande wa soka.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited