Home Soka Coutinho,Trippier watua epl

Coutinho,Trippier watua epl

by Dennis Msotwa
0 comments

Harakati za usajili kwa dirisha dogo la majira ya baridi nchini England zimeendelea baada ua hii leo kufanyika kwa sajili mbili kubwa ndani ya lvilabu viwili vinavyoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo.

Usajili wa mapema ni ule wa mlinzi wa kulia wa kimataifa wa England na timu ya Atletico Madrid ya Hispania Kieran Trippier akiakamilisha usajili wake ndani ya Newcastle united na kuwa usajili wa kwanza tangu timu hiyo ichukuliwe na matajiri wa Saudia Arabia,dau la paundi milioni 25 na makataba wa miaka minne.

Usajili wmingine ulioshtua wengi ni ule wa kiungo wa kimataifa wa Brazil Philipe Coutinho akijiunga na Aston Villa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu akitokea Barcelona,anaenda kuungana na mchezaji wenzake wa Liverpool Steven Gerard ambaye kwa sasa ni kocha wa timu hiyo.Aston Villa watalipa asilimia 60 ya mshahara wake.

banner

Kwa upande wa Newcastle hawajamaliza kwani wamerudi tena Lille ya Ufaransa kutaka saini ya mlinzi wa kati wa Uholanzi Sven Botman licha ya ofa yao ya awali ya paundi milioni 25 kukataliwa.

Naye kiungo wa Arsenal Maitland Niles amejiunga na AS Roma ya Mourinho kwa mkopo wa hadi mwisho mwa msimu huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited