Kipa wa manchester united David De Gea anajiandaa kusaini mkataba mpya klabuni hapo utakaomfanya kuwa golikipa anayelipwa zaidi duniani.
Mkataba huo mpya wa miaka sita utamfanya kipa huyo kuweka kibindoni kiasi cha paundi 350,000 kwa wiki na kumfanya kuwa moja ya wachezaji wanaolipwa vizuri katika ligi kuu ya Uingereza huku akiongoza kwa makipa wanaolipwa vizuri.
Kipa huyo aliyejiunga na United miaka nane iliyopita pia anapigiwa chapuo la kuwa nahodha wa kikosi hicho baada ya kuwa ndio mchezaji mkongwe zaidi kikosini baaada ya kuondoka Antonio Valencia huku Ashley Young akiwa hana namba ya kudumu klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
De gea alijiunga na united enzi za utawala wa Sir Alex Ferguson na sasa amefanikiwa kuwa moja ya makipa bora zaidi duniani.