Home Soka Dembele,Barca hakieleweki

Dembele,Barca hakieleweki

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa FC Barcelona Ousmanne Dembele huenda akaondoka katika klabu hiyo baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya wa kusalia Camp Nou.

Hali kwasasa ni ya mchanganyiko kati ya pande zote mbili,upande wa Barcelona na wawakilishi wa Dembele.Ikumbukwe mkataba wa winga huyo hatari unatarajiwa kumalizia majira ya joto June mwakani.

Barcelona na wawakilishi wa Dembele walikuwa na kikao siku ya jana lakini mambo hayakwenda vizuri kufikia makubaliano baada ya uongozi wa klabu hiyo kutokuwa tayari kumpa mchezaji huyo kiwango kikubwa cha mshahara anachohitaji ili akubali kuongeza mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake huko Cataluna,Hispania.

banner

Klabu bado inataka kujaribu tena kukaa kwenye meza ya majadiliano na wakala wa mchezaji huyo Mousa Sisoko ili kufikia muafaka lakini Dembele hajfurahishwa na hilo.

Upande wa nyota huyo haujafurahishwa na mipango ya klabu hiyo iliyotoka kumsajili Mhispania Ferran Torres hivi karibuni,kwani inaona kama Barca hawawapi kipaumbele huku wakiwa kwenye mipango zaidi ya kusajili wachezaji wapya.Tayari vilabu viwili kutoka Uingereza vimewasiliana na wakala wa mchezaji huyo,vikiwa tayari kumlipa mshahara anaotaka na kumsajili bure mkataba wake utakapoisha rasmi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited