Home Soka Deo Kanda atua Mtibwa

Deo Kanda atua Mtibwa

by Sports Leo
0 comments

Winga wa zamani wa vilabu vya TP Mazembe na Simba sc Deogratius Kanda amejiunga rasmi na wakata miwa kutoka Turiani Morogoro Mtibwa Sugar katika dirisha hili dogo la usajili.

Deo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu ndani ya klabu hiyo huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine endapo ataonesha kiwango kizuri hapo baadae na kuwavutia viungiozi wa klabu.

Wakala wa mchezaji huyo alizungumza na vilabu kadhaa nchini,lakino ofa nzuri kutoka Mtibwa ikiambatana na jinsi gani itavyomtumia mchezaji huyo ndivyo vilivyowashawishi kukubali dili hilo licha ya ukweli kuwa timu hiyo bado inasuasua kupata matokeo kwenye ligi soka soka ya NBC inayoendelea.

banner

Mtibwa inataka kulitumia vizuri dirisha hili la usajili ili kukiimarisha kikosi hicho hasa eneo la ushambuliaji ambalo limekuwa butu sana,hivi karibuni klabu hiyo ilikuwa ikifanya mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Waziri Junior lakini hawakufikia makubaliano ya kusaini mkataba baada ya mchezaji huyo kuwakatalia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited