Kipa namba moja wa klabu ya Yanga Sc raia wa Mali, Djigui Diarra amerejea nchini sambamba na kuingia kambini mapema ya leo akitokea Katika majukumu ya timu ya taifa ya Mali iliyokuwa inashiriki Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
Diarra na timu yake ya Taifa walitolewa katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa 2-1 na wenyeji Ivory Coast ambapo kipa huyo alionyesha kiwango kikubwa katika michuano hiyo akiwa kama kipa namba moja wa timu ya Taifa.
Kurejea kwa kipa huyo kutaiboresha safu ya golini inayochezwa na Abdutwalib Mshery na Metacha Mnata anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara waliocheza dhidi ya Tanzania Prisons.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kipa huyo mpaka sasa amepata cleansheet tano katika michezo aliyocheza ya ligi kuu nchini Tanzania kabla ya kusimama na kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Mali kwa ajili ya michuano ya Afcon 2024.