Tume ya ushindani wa kibiashara Tanzania(Fcc) imejibu shutuma zilizotolewa na Bilionea Mohamed Dewji anayetaka kuwekeza katika klabu ya Simba sc.
Fcc imekanusha taarifa za kuchelewesha mchakato wa kupitia taarifa mbalimbali za uuzaji wa klabu hiyo kwa Bilionea huyo anayedaiwa kutaka kuwekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 20 za kitanzania.
Katika Taarifa yake kwa umma tume hiyo imebainisha kwamba imekua ikipata mrejesho mdogo kutoka kwa klabu hiyo na tayari imeshawapatia mrejesho ambao wanatakiwa kujibu ili kuendelea na hatua zingine za mchakato huo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hivi karibuni wakati akiongeza na waandishi wa habari bilionea huyo Mo dewji aliulizwa kuhusu mchakato huo ulipofikia na alijibu kwamba umekwama katika Tume hiyo ambayo ilipewa ili kuupitia na kuudhinisha.