Shrikisho la soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya makocha ambao hawaruhusiwi kukaa katika benchi la ufundi katika michuano ya klabu bingwa na ila ile ya kombe la shirikisho kutokana na kukosa sifa zinaruhusiwa kikanuni.
Kwa mujibu wa kanuni za CAF makocha wakuu wanapaswa kuwa na leseni ya CAF A kwa wale waliosomea ndani ya Afrika pamoja na UEFA pro license kwa wale waliochukua mafunzo ya ukocha barani Ulaya.
Kocha wa Simba sc Didier Gomez ana leseni ya UEFA A hivyo hana sifa za kukaa katika benchi kwa mechi zilizo chini ya CAF,Simba pia itamkosa kocha wake msaidizi Suleiman Matola ambaye hana leseni ya CAF B inayomuwezesha kuwepo kwenye benchi la ufundi.
Makocha wengine waliopigwa marufuku hiyo ndani ya Afrika Mashariki ni pamoja na kocha wa KMKM ya Zanzibar Ame Khamis,kocha wa APR ya Rwanda Erradi Mohamed Ali,Bosa Wasswa wa Express Fc ya Uganda.