Home Soka Goretzka kitanzini Bayern hadi 2026

Goretzka kitanzini Bayern hadi 2026

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Ujerumani na Bayern Munich Leon Goretzka amesaini nyongeza ya mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kukipiga katika viunga vya Bavaria hadi 2026.

Kiungo huo mkataba wake wa sasa ulikua unaisha mwaka 2022 kulikuwa na wasiwasi wa kuendelea kukupiga kwa mabingwa hao wa Ujerumani baada ya kuhitaji mshahara mkubwa.

Katika dirisha lililopita la majira ya joto Goretzka aliwindwa na vilabu vya Manchester United,Juventus na Real Madrid baada ya kusuasua kwa mazungumzo ya mkataba mpya hali iliyopelekea Bayern kumsjili nahodha wa RB Leipzig Marcelo Sabitzer kama kujiandaa endapo ingempoteza kiungo huyo.

banner

Goretzka ni mmoja kati ya bora wa kati kwasasa duniani na pacha yake na Mjerumani mwingine Joshua Kimmich inatajwa kama pacha bora zaidi kwa ubora barani Ulaya.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited