Mashabiki wa Yanga hawana budi kutembea kifua mbele baada ya mdhamini wa klabu hiyo kampuni ya Gsm kurejea mazima kuisaidia klabu hiyo.
Inaelezwa kampuni hiyo tayari imeshaaanza kushughulikia mambo kadhaa tangu kurejea kwake kama ujenzi wa uwanja wa mazoezi kigamboni ambao utaanza kutumika msimu ujao huku pia ikiendelea na mchakato wa kusaidia mabadiliko ili kuenda kwenye mfumo wa hisa.
Pia kampuni hiyo inaendelea na mchakato wa usajili ambapo inatarajiwa kushusha majembe ya maana kutoka nje ya nchi ili kuboresha kikosi hicho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.