Kiungo Matteo Guendouz ameaga katika klabu ya Arsenal akienda kukamilisha kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu nyingine baada ya muda wake wa mkopo katika klabu ya Hertha Berlin kumalizika.
Inadaiwa mchezaji huyo yupo mbioni kujiunga na Marseille ya nchini Ufaransa huku akisubiri kukamilisha vipimo vya afya na alitumia mitandao yake ya kijamii kuandika ujumbe wa kuaga katika klabu hiyo ambapo ujumbe huo ulisomeka kama ifuatavyo japo aliwahi kuufuta.
“Nimegundua na kujifunza mengi nikiwa hapa, ni ngumu kutaja kila kitu lakini sitosahau dakika hata moja nikiwa na jezi ya Gunners”
“Sitosahau dimba la Emirate, sitosahau mashabiki..na sitosahau hili jiji..sitosahau kila nilichopitia hapa..sitosahau kuwa lengo langu lilikua kuipigania rangi ya Arsenal”
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Ahsante kwa wote walioniamini nikiwa Arsenal, wakati wa mazuri na mabaya..naitakia mafanikio timu na mashabiki wanaostahili matokeo mazuri mno..mniamini..Kwaheri Arsenal na nitakua Arsenal (Gunner) milele.”
Mchezaji wa Arsenal Matteo ama Matayo Gueondouzi ameandika barua ya kuwaaga Arsenal.