Mwili wa aliyekua mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Simba na mjumbe wa kamati ya maadili ya TFF Zacharia Hans Poppe umeagwa mchana huu na wadau mbalimbali wa michezo hapa Tanzania katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Hanspoppe alifariki siku ya Jumamosi alipokua hospitali akipatiwa matibabu ya matatizo ya kupumua.
Zacharia atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa klabu yake pendwa ya Simba kwa kuwa mmoja wa waandamizi walioiwezesha klabu hiyo kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi kwa miaka ya hivi karibuni,pia atakumbukwa katika mchango wake kwenye maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.
Baada ya kuagwa jijini Dar es salaam mwili wa mfanya biashara huyo maarufu utasafirishwa kwenda kwao Iringa kwaajili ya mazishi.
Mungu ailaze roho yake,mahali pema peponi,Amin