Klabu ya Namungo FC itakayoshiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) imevunja mkataba na kocha wake Hitimana Thiery raia wa Burundi kwa makubaliano ya pande zote mbili na Kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Hemedi Morocco kutoka Zanzibar.
Namungo ilifanikiwa kumaliza ligi kuu katika nafasi ya nne msimu uliopita huku ikifanikiwa kufika fainali ya michuano ya Azam Sports Confederation Cup ambako ilifungwa na Simba sc lakini ilibahatika kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa katika kombe la shirikisho baada ya Simba sc kutwaa taji la ligi na F.a hivyo kanuni kwapa nafasi Namungo Fc.
Kocha Hemed Morocco atakua na kibarua cha kuhakikisha timu hiyo inarejea katika ubora wake baada ya kumpoteza nyota wake Reliants Lusajo aliyejiunga na Kmc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.